bajeti
Bajeti ni makadirio ya kipato na matumizi ya Asasi ndani ya kipindi cha muda fulani.
Vidokezo vya kuweka bajeti:
- Taja kila vipengele vya kipato na matumizi kwenye mpango wako.
- Fanya utafiti kwenye bei halisi kwa kila gharama.
- Linganisha bei kutoka kwa wauzaji wengine ili kuhakikisha unapata bei nzuri.
- Jiandae kuendana na bajeti kama vitu havitaenda kama ilivyopangwa kwenye mpango, baadhi ya gharama zinaweza kuondolea au kubadilishwa ili kuhakikisha kuwa matumizi yako sawa na kipato.
kutafuta pesa
Kutafuta pesa ni kule kuomba msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia mpango wako. Kuna aina kuu mbili za kutafuta pesa, kutafuta pesa kwa njia rasmi na kusiko rasmi. Kutafuta pesa kwa njia rasmi kunaweza kuwa kama ruzuku.
Vidokezo vya kukusanya pesa kiufanisi:
- Kuwa na bajeti wazi, taja kila kipengele cha kipato na matumizi.
- Anza ukusanyanji pesa wako kwa watu walio karibu yako, familia yako na marafiki.
- Waulize walimu na viongozi wakusaidie.
- Omba msaada wa kifedha kwa wadau ambao wanahamu na kitu unachokifanya, na watanufaika kitu fulani kutoka kwenye mpango wako.
- Wajibika na kuwa mwaminifu katika ukusanyaji wako wa pesa. Rudisha mrejesho kwa wafadhili wako unaoonesha kiuhalisia ni wapi pesa zao zimeenda.
- Onesha moyo wa shukurani na kujali kwa wafadhili wako.