Licha ya ukweli kwamba vijana wanakuwa na mawazo ya ujasiri katika kuweka mipango kwenye jamii zao, utafiti wetu unaonesha kwmba vijana mara zote hawajui wapi pa kuanzia kutekeleza mawazo yao. Katika ukurasa huu unaweza kupata ushauri namna ya kupanga utekelezaji wa mipango yako.
Kupanga ni nini?
Kupanga ni maandalizi sawa kwa hatua ambazo zitakusadidia kufikia malengo yako. Mpango ni kama kuwa na ramani ya mipango yako yote.
Kwanini kupanga ni muhimu?
Kupanga kutakusaidia:
- Tambua kwa makini maono yako ya muda mrefu, na yale ya muda mfupi.
- Weka wazi matatizo yako ambayo utaweza kukumbana nayo njiani na elezea jinsi utakavyo weza kuzitatua changamoto hizo.
- Fuatilia mafanikio yako kwa kufuata maendeleo ya malengo yako.
Namna ya kupanga
- Tambua malengo yanatakiwa kufikiwa. Kwanza, weka maono ya mpango wako, ni nini unachojaribu kufikia. Jaribu kuvunja malengo yako katika malengo ya muda mfupi. Weka kipaumbele katika malengo hayo kwa kuangalia nini kinachotakiwa kufikiwa kwanza.
- Tambua wadau muhimu
- Tengeneza mikakati na namna utakavyofanya ili kufikia kila lengo, fua.ta kila hatua ndogo.
- Panga jinsi utakavyopata au nufaika na mbinu zinazohitajika, hii ni pamoja na fedha, wafanyakazi, muda na rasilimali taarifa.
- Tambua matatizo yeyote muhimu na vitu ambavyo zinatakiwa kutatuliwa, na jinsi ya kurudia mpango ili kuweza kuendana na mpango ya kutatua matatizo hayo.
- Tengeneza ratiba ya mradi. Tambua kazi na wajibu uziweke kwa kila muhusika wa kikundi.
- Weka tarehe ya lini kila lengo au kazi inatakiwa ikamilike.
- Wasilisha mpango kwa wadau na fanya mabadiliko muhimu watakavyotaka.
- Tekeleza mpango wako huku ukiendelea kufuatilia kama hatu zote za mpango mkakati wako ili kuhakikisha zinakuwa zimetekelezwa katika mtiririko unaotakiwa.