Career Hub inatoa huduma tano tofauti ndani ya sehemu ama eneo lake maalum.
Ushauri
Ushauri utafanyika ktk vikundi vya watu wengi, na kwa kawaida itakuwa mashuleni. Katika vikao hivi tunalenga kukusaidia utambue uwezo (nguvu) wako, udhaifu (mapungufu) yako na ujuzi uliyonao. Halafu tutakuwezesha kuoanisha ujuzi huo na njia ya kuendea fani inayokufaa. Katika vikao hivi tunatumia wigo mpana wa mbinu za kuingia katika soko la ajira, Taasisi za elimu ya juu, kuhahakisha kwamba, wanafunzi wanazingatia njia zote kadri inavyowezekana kuishi fani zao kwa baadae. |
Mafunzo ya fani (Kazi)
Mafunzo ya fani ni vikao baina ya watu wawili mfindishaji na anayefundishwa. Hufanyika katika ofisi zetu za Career Hub. Wakati wa vikao hivi, wakufunzi wetu watawawezesha vijana kufata machaguo yao ya fani( kazi) kwa ufanisi kadri inavyowezekana. Hii itafanyika kupitia vikao vya kuendeleza ujuzi, ushauri juu kufanya maombi, na taarifa sahihi juu ya fulsa zilizopo kwenye sekta uliyochagua katika maombi yako. |
Mashauriano kwa mipango ya wanafunzi
Tunafahamu kwamba kupanga kuanzisha jambo/Mpango mpya ni ngumu. Katika mashauriano ya namna hii, tunatoa vyanzo vikuu viwili kufanya mpango wa wanafunzi kufanikiwa. Tutakusaidia kupata vyanzo vya takwimu husika kuunga mkono mpango wako wa wanafunzi. Pia tutatoa ushauri wa namna ya kutafuta fulsa za msaada. |
Vikao vya uwezeshaji
Vikao vya uwezeshaji vitaandaliwa ndani na Career Hub, na kutangazwa katika mitandao ya kijamii na orodha ya barua pepe. Vikao hivi vitawapa vijana uwanda mpana wa maelezo kwa ujumla wake kuhusu kipengele fulani cha fani iliyoshauriwa. Hapo nyuma, vikao vya uwezeshaji vilijumuisha juu ya ajira na uelekeo wa kuchagua fani kwa wanafunzi ambao bado hawajajiunga na vyuo. Jiunge kwenye orodha ya barua pepe ili kupata taarifa za vikao vijavyo mbeleni. |