Uzoefu wa kazi ni nini?
Ikiwa mtu amefanya kazi katika taaluma yake kwa muda mlefu, huchukuliwa kama mfanyakazi mwenye uzoefu. Uzoefu wa kazi huendeleza ujuzi, huongeza maarifa na kumfanya mtu kujifunza utamaduni wa kazi katika nyanja husika. Uzoefu wa kazi husaidia vijana kuwa na sifa za zaidi na ziada kuomba ajira. Waajiri hupendelea kuajiri watu wenye uzoefu wa kazi kuliko wahitimu wenye mafunzo ya nadhari, huwa hawana ufanisi kazini.

Unapataje uzoefu?
Kuna aina kuu mbili za kupata uzoefu wa kazi kwa wahitimu wapya wa masomo: tarajali na kujitolea.
Tarajali ni kipindi ambapo wahitimu hufanya kazi chini ya uangalizi katika shirika ama kampuni fulani kwa kipindi cha muda fulani. Hii njia safi sana ya vijana wahitimu wapya kupata uzoefu kazini. Unaweza kuwa unalipwa ama lah!
Kujitolea ni kitendo cha kujitoa, kutoa muda wako, nguvu na ujuzi ulionao kutoa huduma kwa jamii bila kutegemea malipo. Ni njia mojawapo ya wahitimu wasiokuwa na uzoefu wa kazi kujipatia uzoefu wa kazi. Husaidia kugundua changamoto zinazoikumba jamii na kuendeleza ujuzi wa kutatua matatizo.

Faida za uzoefu wa kazi:
Husaidia kufanya ramani maisha yako ya kazi. Kupata uzoefu katika nyanja husika uliojifunza darasani, Husaidia kufahamu ni kazi gani unapaswa kujikita. ·
Inakuongezea mtandao wa watu wataalamu katika taaluma yako. Kufanya kazi katika shirika linalotambulika inasaidia kufungua milango kwa taraji kuwa na mahusiano na watu wengi wataalamu. Kwa kuhudhuria vikao, semina na kupitia kazi pia hukutana na watu wapya, ambapo huwezi jua ukapata bahati ya kupata kazi ya ndoto zako.
Inakusaidia kutengeza wasifu mzuri. Wasifu ulioshiba ni kigezo muhimu katika kupata ajira. Uzoefu wa kazi unakupatia maudhui ya kuandika wasifu wako mzuri na barua ya maombi.
Inajenga ujuzi wa kitaalamu katika kazi. Kupitia uzoefu wako unajenga hali ya kujiamini, na uelewa wa mazingira ya kazi kitaalamu. Lakini huendeleza ujuzi kama vile kufanya kazi kwa umoja, kujali muda, mawasiliano na ujuzi binafsi.
· Inatoa motisha na kukupa nguvu ya kufanikiwa malengo yako ya kitaalamu. Kwenda kazini kila siku, kukutana na wafanyakazi na wateja na wataalamu wengine wabobevu kunatoa mwanya wa kupata mitazamo chanya. Itakupa nguvu ya kuendelea kukaa kwenye mstari na kujenga ari ya kufanya kazi ya ndoto yako.

Kwa nini Uzoefu wa kazi ni muhimu?
Uzoefu wa kazi huongeza ufanisi na matokeo kazini. Kuajiri mtu mwenye uzoefu wa kazi, waajiri hutegemea kuwa na mtu mwenye maarifa na uzoefu katika mazingira ya kufanya hizo na hivyo kufanya majukumu kwa kiwango kikubwa. Hii hufanya taasisi kuwa na ushindani na taasisi zingine na kutoa mafanikio. Inaongeza pia nafasi ya kupata ajira Mahali pengine.