Vidokezo
Umeshatuma wasifu wako na barua ya maombi kwa ajili ya maombi na umeshafanikiwa, umeitwa kwa ajili ya usaili. Jinsi utakavyojiandaa kwa ajili ya usaili itaonesha mafanikio yako katika kupata kazi. Katika ukurasa huu tunatumaini kuwa, utajifunza mbinu ambazo zitakusaidia kufanya vizuri katika usaili wako.
Vidokezo vikuu vya kufanikisha usaili:
- Siku chache kabla ya usaili, jaribu kutabiri maswali ambayo utaulizwa kwenye usaili. Andika maswali ambayo ni lazima uulizwe kwa mfano, “kwanini tukuajiri wewe?”
- Fanya utafiti juu wa shirika hilo ili kuweza kuwa na taarifa kuhusu shirika. Hii itaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya kazi ambazo zinafanywa na hilo shirika, umuhimu na maelekezo mengine muhimu ambayo yatakusaidia kuwa na uelewa zaidi.
- Rudia kusoma tena maelekezo ya kazi. Soma majukumu ya kazi, maarifa na ujuzi ambao waajiri wanaangalia. Unapokuwa unajibu maswali, husianisha na kile ambacho muajiri anahitaji kutoka kwenye ujuzi na uzoefu wako.
- Mazoezi hufanya ukamilifu. Fanya mazoezi katika kujibu maswali na fanya mazoezi pia ya usaili pamoja na marafiki au familia yako. Hii itaweza kukusaidia kuimarisha ujasiri wako.
- Andaa maswali ya kuuliza, mara nyingi muhojiwa atapewa nafasi ya kuuliza maswali, angalia zaidi kile ambacho unahitaji kujua kuhusu kazi. Swali la kuuliza linaweza kuwa: ni changamoto gani kwa sasa zinayoikumba zaidi nafasi ya kazi ninayooomba?
- Jiamini. Kabla ya kipindi cha usaili kuanza kunywa maji, vuta pumzi ndefu ili kuondoa woga na jihakikishie wewe mwenyewe kuwa utafanya vizuri.
Vidokezo vya vitendo
- Wahi kufika. Hakikisha umefika eneo la usaili hata nusu saa au lisaa kabla ya muda wa kuanza usaili. Panga safari na usafiri wako kabisa.
- Fikiria kazi unayoitaka, halafu uvae ipasavyo kwa ajili ya usaili.
- Uonekane vizuri, safisha viatu vyako, hakikisha nguo zako ni safi, chana nywele zako, na hakikisha kucha zako ni safi.