Maelekezo ya Kazi
Katika sekta ya Kilimo, kuna aina kuu tatu za majukumu: Kulima, meneja wa kilimo, na mshauri wa kilimo.
Majukumu ya kila siku ya wakulima yanajumuisha:
Meneja wa Kilimo mara nyingi pia hushiriki katika shughuli za ulimaji, lakini pia anachukua nafasi katika biashara ya mashamba kwa:
Wataalam na washauri wa kilimo kwa ujumla wanafanya kazi zaidi ya vitengo vyao, kwa kubuni maboresho ya sekta ya kilimo. Kazi hizo ni pamoja na:

- Kuchunga kwenye Mifugo au Mazao
- Kulima
- Kupanda na Kuvuna mazao
- Kufanya marekebisho na matengenezo ya magari, zana za kulimia, uzio, mageti na ukuta
Meneja wa Kilimo mara nyingi pia hushiriki katika shughuli za ulimaji, lakini pia anachukua nafasi katika biashara ya mashamba kwa:
- Kuwasimamia wafanyakazi wa shamba.
- Kufuatilia mipango fedha.
- Kupendekeza na kuleta mikakati ya kuvuna au kupanda mbegu.
- Kutembelea masoko ya wakulima na wauzaji wa nafaka.
Wataalam na washauri wa kilimo kwa ujumla wanafanya kazi zaidi ya vitengo vyao, kwa kubuni maboresho ya sekta ya kilimo. Kazi hizo ni pamoja na:
- Kutafiti na kutambua matatizo makuu ili kuboresha mazao ya kilimo.
- Kuimarisha uwezo wa vikundi vya wakulima ili kuimarisha uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya mashaba.
- Kupanga, kufuatilia na kutekeleza miradi kwenye mashamba na kuongeza maeneo zaidi.
- Kuwaelimisha wakulima.
Ujuzi Stahiki
Kufuata kazi katika kulima na kusimamia shamba kwa ujumla, ni muhimu kuwa na ujuzi ufuatao:
Wataalamu na washauri wa kilimo zaidi sana wanatakiwa wawe na ujuzi ufuatao:

- Maadili ya hali ya juu katika utendaji na utayari wa kufanya kazi muda mrefu.
- Ukakamavu wa kimwili na nguvu.
- Ujuzi wa mitambo na uwezo wa kutengeneza mashine na vifaa.
- Ujuzi wa kufanya kazi kwa pamoja.
- Moyo wa ujasiliamali na uwezo wa kupanga na kusimamia mauzo.
Wataalamu na washauri wa kilimo zaidi sana wanatakiwa wawe na ujuzi ufuatao:
- Ujuzi katika uchambuzi na utoaji wa taarifa.
- Uwezo wa kutatua changamoto.
- Ujuzi wa kuandika na kuongea katika lugha ya Kiswahili na Kingereza.
- Umakini na ubunifu pamoja na uwezo wa kufanya kazi chini ya usimamizi mdogo na ukaoata matokeo na majawabu.
- Ujuzi katika mitandao ya kijamii, pamoja na uwezo wa kushirikiana na serikali, sekta binafsi na Asasi za kiraia.
Mahitaji
Wakulima na wasimamizi wa mashamba hawana ulazima wa kuwa na vigezo vya kitaaluma, lakini watafaidika kwa kuwa na uzoefu katika kazi. Ili kupata nafasi katika ushauri wa kilimo, waajiri kiujumla huitaji shahada ya kwanza katika teknolojia ya kilimo au shahada inayoendendana. Zaidi ya hayo, waajiri pia wanaangalia uelewa wa mabadiliko katika vikundi vya uzalishaji, mabadiliko katika masoko ya ndani, usindikaji wa kilimo na masoko.