Kwa nini kupanga kwa Uendelevu?
- Vyanzo vingi vya msaada ambavyo husaidia mipango ya wanafunzi kwa uhalisia ni vya muda mfupi. Utahitaji mipango endelevu ili kuhahakisha mipango yako haikwami mara mzunguko mmoja wa msaada unapokoma.
- Utahitaji kuwa umepanga namna gani mipango yako itadumu katika muda wote wa mabadiliko ya kisiasa, uchumi na mazingira ya watu.
- Ni muhimu jamii isipoteze Ubora wa programu, kwa sababu tu ilishindikana kuzingatia kuifanya endelevu.
Mpango endelevu utakuwa:
- Utoe dira/mtizamo unaoleweka katika mpango wako.
- Kuweka mikakati ya muda mlefu.
- Kulinganisha na mipango mingine ili kupima maendeleo yake
- Kuonesha thamani ya mpango kwa wadau
Tabia kuu za uendelevu
- Dira/mtizamo. Weka Dira inayoeleweka ambayo itakuwa inalenga mpango wako mzima. Ni kitu gani hasa unachotaka kuendeleza katika jamii.
- Matokeo. Weka vizuri malengo pamoja na vishiria vya kupima ufanisi, na oanisha na tarehe husika ili uwe unaangalia maendeleo yake.
- Kuwa na mikakati ya fedha. Pima mahitaji yako muhimu ya muda mlefu. Tafiti vyanzo vyako muhimu vya mapato, na ufanye mipango yako ya muda mlefu kwa namna utakavyo endeleza kutafuta misaada.
- Kuendana na hali ya mabadiliko. Panga mipango kwa namna utakavyoendana na mpango wako katika hali tofauti za uchumi, siasa na hali ya watu kufanya vizuri.
- Msingi mkubwa wa msaada wa jamii.
- Wadau wakuu. Tengeneza mpango wa kuwa na Wadau wakuu. Fanya tafiti kwa upana wa wadau kama vile vikundi vya wanafunzi, marafiki na walimu.
- Mfumo imara wa ndani. Wagundue wafanya maamuzi wakuu na kuhakikisha una watu wakusimamia shughuli muhimu za mpango, kwa mfano Muhasibu, Afisa wa utawala na rasilimali.
- Mpango endelevu kwa ujumla ambao utazingatia mahitaji ya muda mfupi na muda mlefu. Gundua changamoto muhimu na rasilimali utakazotumia kutatua changamoto hizo.