Kujitolea ni nini?
Kujitolea ni kujitoa nguvu zako, muda wako na kutumia ujuzi ulionao na maarifa yako kusaidia jamii bila kulipwa fedha. Baadhi ya shughuli zinazofanywa na watu wanaojitolea ni kufundisha, ujenzi wa vyoo, usafi wa mazingira na shughuli nyingine nyingi.
Aina za kujitolea
Zipo aina kuu mbili za kujitolea: Kujitolea katika mfumo ulio rasmi na mfumo usio rasmi:
Mfumo rasmi: Huu Hufanyika kupitia mashirika yaliyojisajiri kisheria na mfumo rasmi wa kujitolea, maranyingi ni mashirika yasiyo kiserikali lakini pia taasisi za kiserikali na taasisi binafsi. Kunakuwa na mikakati ya mipango maalum na muda muafaka wa kujitolea. Kwa mfano Cambridge Development Initiative, VSO na Raleigh ni mashirika yakimataifa yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na kujitolea ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii na kusaidia kufanikiwa kwa mpango wa maendeleo endelevu wa Dunia.
Kujitolea kwa mfumo usio rasmi hufanywa na watu tu bila kuwa na shirika ama taasisi maalum. Ni vikundi vya watu ama mtu mmojammoja ambao huamua kutumia nguvu zao, ujuzi na maarifa waliyonayo kusaidia watu kwa kutatua changamoto katika jamii.

Watu hujitolea wapi?
Kujitolea katika mfumo rasmi, hufanyika kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi, mashirika ya umma na asasi mbalimbali za kijamii. Miradi mbalimbali inayofanywa ni pamoja na; Miradi ya, elimu, afya, tafiti na miradi mingine ya maendeleo ya jamii. Watu hujitolea Duniani kote, katika nchi zao ama kwenda mataifa mengine. Katika mfumo usio rasmi watu hujitolea popote.

Kwa nini watu hujitolea?
Kujifunza na kuendeleza ujuzi
"I decided to volunteer with Kite because I believe it is a good platform for me to be able to reach out to my society. And also it lets me do that along with my practical training period and hence increase my skills too!"
- Jackline Chris a volunteer for KITE Dar es Salaam
Kurudisha shukrani kwa jamii na wengine kumshukuru Mungu.
"I chose to spend my summer volunteering for CDI Education because I felt that education is as universal human right, and that all children, regardless of their race, ethnicity, gender, sexual orientation, and/or socioeconomic status, deserve fair and equal access to schooling." -
Priyanka, a volunteer from Cambridge Development Initiative (CDI), Summer 2018.
Kupata ujuzi na Kujiongeza thamani katika kazi. Baadhi ya taarifa nyingi zinaonyesha wahitimu wa vyuo vikuu hawana uwezo wanapoajiriwa. Hivyo kujitolea hufanya vijana kujifunza, kupata uwezo na kupata uzoefu kwenye kazi zao walizosomea.
"I decided to volunteer because I wanted to fill my summer with something productive whilst gaining skills and actually making an impact."
Aditi, a volunteer from Cambridge Development Initiative (CDI), Summer 2018.
Kupata ujasili, kukutana na vijana wengine, na kufurahia pia. Kujitolea kunakukutanisha na watu wapya wenye tamaduni na asili tofauti. Ukiachilia kazi, ni sehemu ya kufurahia mambo mengi sana.
"I decided to volunteer this year as to return to the society the parts of the things I have learning for all these years and to bring positive change to the society I can reach. Volunteering to me is like thanksgiving to my almighty living God who has given me strength to overcome all the obstacles, hurdles to complete my very race in the award of Bachelor Degree. I always feel honored and blessed to serve my society and country as large." - Geofrey KITE Volunteer 2018
Kufanya mabadiliko chanya kwa jamii.
Ili kujitolea unahitajika kuwa na:
Uwe huru na uwe na uwezo wa kukabiliana na mazingira mapya. Unatarajiwa kuishi kwenye utamaduni mpya kabisa, kukutana na vyakula vya aina mpya na mtindo mpya wa maisha. Uweze kujitegemea na kuwa na mipango binafsi, maana huwezi kuwa chini ya uangalizi muda wote. Lakini pia, uwe tayali kutoa kuliko kupokea.
Umuhimu wa kujitolea:
Kujitolea ni njia ya kuongeza uzoefu wa kazi na kufungua njia ya kazi ya mtu aliosomea. Moja ya changamoto kubwa kwa wahitimu ni kukosa uzoefu stahiki ambao waajiri huutaka. Ili kupata uzoefu huo kujitolea ni njia mojawapo inayotoa fursa kwa vijana kupata uzoefu huo.
Pia ni njia ya kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko katika jamii. Hutoa fursa ya kushiriki moja kwa moja kuleta mabadiliko katika jamii ikiwa ni pamoja na kufanikisha mpango wa maendeleo endelevu.
Kujitolea ni njia ya kutoa elimu, ni njia ya kueneza upendo, ushirikiano, amani na furaha kwa watu wengine ndani ya jamii.

“Volunteerism is a powerful means of engaging people in tackling development challenges, and it can transform the pace and nature of development. Volunteerism benefits both society at large and the individual volunteer by strengthening trust, solidarity and reciprocity among citizens, and by purposefully creating opportunities for participation”. - United Nations Volunteer