Barua ya kuonesha hamasa ni nini?
Barua hizi mara nyingi hutumika katika nafasi za elimu, kazi za kujitolea na miradi mbalimbali. Barua za kuonesha hamasa ama sifa zako hutofautiana na barua za maombi, kwani mara nyingi hazitumiki kwa maombi ya kazi. Barua za namna hii hutoa nafasi ya kujieleza kwanini umevutiwa na shughuli fulani, ueleze uwezo wako na kuonesha kwa nini wewe ndo chaguo sahihi katika nafasi hiyo.
Vidokezo muhimu vya kuandika barua ya namna hii vizuri:
- Barua yako ijieleze vizuri.
- Elezea haja yako kwenye hiyo nafasi, na onesha mfano wa kitu ulichofanya. Kwa mfano elezea kwa nini unataka kusoma shahada ya pili ya mambo fulani katika chuo fulani.
- Eleza kwa undani unaomba nini na una mategemeo gani katika shughuli hiyo.
- Tumia lugha nyepesi, usifanye mambo magumu sana.
- Taarifa zako zote ziwe za kweli.
- Epuka makosa ya herufi na makosa ya kisarufi. Soma barua yako baada ya kuiandaa na umpe mtu mwingine asome na kukusahihisha.