Kabla hujaamua kazi ipi itakufaa, Inatakiwa Kwanza kutambua wewe ni Mtu wa aina gani, nguvu, udhaifu, ujuz na Nini Unataka Njema ya kazi.
Wewe ni mtu wa aina gani?
Kwanza kabisa, katika ugunduzi binafsi ni muhimu kujitambua wewe ni mtu wa aina gani,ili ufanye kazi kuelewa nguvu na udhaifu wako. Jaribu kipimo hiki cha Mwonekano:
|
|
Kitu kipi kinakufurahisha?
Ili kutambua ni kitu gani Unapenda kukifanya,ni vizuri kuyagawa maisha yako katika vipengele, kama vile: Kazi, Mafunzo, familia, ujuzi na starehe.
Zingatia na weka Kumbukumbu ya maswali yafuatayo.
Kazi
Mafunzo
Ujuzi
Burudani
Zingatia na weka Kumbukumbu ya maswali yafuatayo.
Kazi
- Ulitaka kufanya nini wakati ulipokuwa mdogo?
- Unataka kufanya nini sasa?
- Kwa nini imebadilika?
Mafunzo
- Ni masomo gani uliyochagua ambayo unafurahia kujifunza?
- Ni sehemu ipi umejikuta inakuvutia mno?
- Upo vizuri sana kwenye ujuzi gani? Kwa mfano, kuandika vizuri, kutatua matatizo, ujuzi wa kompyuta
Ujuzi
- Ni ujuzi gani ambao tayali unao?
- Ni ujuzi upi unafurahia kujiendeleza zaidi?
Burudani
- Unapenda kufanya nini kama burudani
- Ni kitu gani unapendelea kufanya zaidi ya kingine?
Una uwezo kwenye mambo gani?
Kufahamu uwezo wako ni zaidi ya kujua kitu gani unapenda kufanya, unapswa kuzingatia ni vitu gani unafurahia na ni wapi vinaingiliana na vile unavyoviweza.
- Kwanza zingatia vipaji vyako. Fikiria vitu unavyoviweza kwa uhakika, hata kama hutaki kuvifanya, jaribu kufahamu ni ujuzi gani unaotumia kufanya shughuli hizo.
- Waulize rafiki zako na familia yako wakueleze, wanafikiria uko vizuri kwenye nini na uko vibaya kwenye mambo gain. Wahimize waseme ni wakati gani maalum ulikuwa vizuri na wapi ulikuwa vibaya.
- Fikiria kwamba, ni wakati gani kwa mara ya mwisho ulihisi ulikuwa vizuri. Ni kitu gani hasa wakati huo ulikifanya kwa usahihi?
Unapimaje mafanikio?
Kabla hujachagua njia ya fani/kazi, ni lazima ufikirie kuhusu thamani yako na nini hasa unakitaka katika maisha. Jaribu kufikiria na kufahamu una ndoto gani katika mlengo wa fani au kazi yako. Fikiria kuhusu maswali hay a:
- Unathamini nini?
- Kitu gani kinakupa hamasa? Ni wakati wa shughuli gani hujihisi unashiriki vyema na mwenye nguvu kuzifanya?
- Vitu gani unavipa vipaumbele kwenye Vitu unavyovitaka katika maisha? Kwa mfano; kuendeleza familia yako, kusaidia maendeleo ya jamii n.k.
- Fikiria kuhusu watu unaowaheshimu; Unataka watu waseme nini kuhusu wewe?
- Kama pesa ingekuwa siyo kikwazo, ungependa ufanye nini?